
Mchezaji kinda Mfaransa Kylian Mbappe na Mwingereza Harry Kane ni miongoni mwa wachezaji walioorodheshwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2018.
Eden Hazard wa Chelsea, Mohamed Salah kutoka Liverpool, Kevin De Bruyne wa Manchester City na mshambuliaji mpya wa Juventus Cristiano Ronaldo https://king360live.blogspot.com/Michezoni miongoni mwa waliojumuishwa.
Lucy Bronze kutoka Uingereza pia amejumuishwa katika tuzo hiyo kwa upande wa wanawake.
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane mwenye miaka 24 alishinda kiatu cha dhahabu baada ya kuibuka mfungaji bora katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi akiwa na magoli 6 na kuifanya England kumaliza nafasi nzuri zaidi katika mashindano haya tokea mwaka 1990.

Alishiriki michuano hii ya kombe la dunia akiwa tiyari na magoli 30
Aliweza pia kuwa na kiwango kizuri katika michuano ya kombe la dunkwenye ligi kuu England.ia, akiwa mchezaji wa kwanza kutoka England kushinda kiatu cha dhahabu tokea alivyofanya Gary Lineker mwaka 1986.
Hazard mwenye miaka 27 alishinda kikombe cha FA akiwa na Chelsea mwezi Mei na pia kuifikisha timu ya Ubelgiji katika nafasi ya tatu kwenye michuano ya kombe la dunia ikiwa ndio nafasi nzuri zaidi kwa Ubelgiji kuifikia tokea kuanza kwa mashindano haya.

Salah mwenye miaka 26 alikua pia na msimu mzuri ndani ya Liverpool. Raia huyu wa Misri alifunga magoli 46 kwa upande wa klabu na kwenye timu ya taifa, huku pia akiifikisha Liverpool katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

Walioorodheshwa
- Cristiano Ronaldo - Juventus & Ureno
- Kevin De Bruyne - Manchester City & Ubelgiji
- Antoine Griezmann - Atletico Madrid & Ufaransa
- Eden Hazard - Chelsea & Ubelgiji
- Harry Kane - Tottenham & England
- Kylian Mbappe - Paris St-Germain & Ufaransa
- Lionel Messi - Barcelona & Argentina
- Luka Modric - Real Madrid & Croatia
- Mohamed Salah - Liverpool & Misri
- Raphael Varane - Real Madrid & Ufaransa
Kwa upande wake De Bruyne mwenye miaka 27 alikua na mchango mkubwa sana katika rekodi nzuri iliyowekwa na klabu yake ya Manchester City kwa kufikisha alama 100 na kuipa ubingwa wa EPL. Alifanya vyema pia akiwa na timu yake ya taifa ya Ubelgiji iliyoibuka mshindi wa tatu kwenye kombe la dunia 2018.
Ulikuwa mwaka mzuri pia kwa mshindi mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo. Mreno huyu alifunga magoli 54 katika michezo 54 ya michuano yote, akiipa pia klabu yake za zamani Real Madrid kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo.
Mwisho wa kupiga kura utakua Agosti 10 na tuzo zitatolewa mjini London Septemba 20.

Kwa upande wa wanawake Lucy Bronze wa England ameorodheshwa baada ya kuwa na msimu mzuri akicheza kama mlinzi wa kushoto.
Bronze mwenye miaka 26 anayechezea Ligi kuu ya Ufaransa ameisaidia Lyon kushinda kikombe cha ligi kuu na kile cha ligi ya mabingwa Ulaya katika msimu wake wa kwanza akiwa na Lyon baada ya kuondoka Manchester City mwezi Agosti.
Walioorodheshwa
- Lucy Bronze - Lyon & England
- Pernille Harder - Wolfsburg & Denmark
- Ada Hegerberg - Lyon & Norway
- Amandine Henry - Lyon & Ufaransa
- Samantha Kerr - Perth Glory/Chicago Red Stars & Australia
- Saki Kumagai - Lyon & Japan
- Dzsenifer Marozsan - Lyon & Ujerumani
- Marta - Orlando Pride & Brazil
- Megan Rapinoe - Seattle Reign & Marekani
- Wendie Renard - Lyon & Ufaransa